Az-Zukhruf 43:35
الزخرفوَزُخْرُفًا ۚ وَإِن كُلُّ ذَٰلِكَ لَمَّا مَتَـٰعُ ٱلْحَيَوٰةِ ٱلدُّنْيَا ۚ وَٱلْـَٔاخِرَةُ عِندَ رَبِّكَ لِلْمُتَّقِينَ
Na mapambo. Lakini hayo si chochote ila ni starehe ya maisha ya dunia tu, na Akhera iliyoko kwa Mola wako Mlezi ni ya wenye kumcha Mungu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na mapambo. Lakini hayo si chochote ila ni starehe ya maisha ya dunia tu, na Akhera iliyoko kwa Mola wako Mlezi ni ya wenye kumchamngu. [35]
[35] Na tungeli wafanyia milango ya nyumba zao na vitanda kuwa ni vya fedha wakineemeka navyo na wakiegemea juu yake. Na tungeli wafanyia mapambo ya kila kitu. Na starehe zote hizo tulizo kusifia si chochote ila ni starehe za kupita njia, ni za uhai huu tu wa duniani. Na malipo ya Akhera mbele ya Muumba wako na Mlezi wako yameandaliwa kwa wanao jilinda na ushirikina, na wakayaepuka maasi ya kuangamiza.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na tukawafanya wawe na dhahabu. Na vyote hivyo havikuwa isipokuwa ni sterehe za maisha ya kilimwengu, nazo ni starehe chache zenye kuondoka. Na starehe za Akhera zimehifadhiwa kwa Mola wako kwa wale wachamungu na si kwa wengine.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net