Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 43 · Aya ya 37

Az-Zukhruf 43:37

الزخرف

وَإِنَّهُمْ لَيَصُدُّونَهُمْ عَنِ ٱلسَّبِيلِ وَيَحْسَبُونَ أَنَّهُم مُّهْتَدُونَ

Maana

Na hakika wao wanawazuilia Njia na wenyewe wanadhani kuwa wameongoka.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na hakika wao wanawazuilia Njia na wenyewe wanadhani kuwa wameongoka. [37]

[37] Na hakika Mashetani wanao jitia upofu na Qur'ani huwazuia na Njia anayo itia Rahmani. Na hao wanao tumiliwa wanadhani kwa kuwafuata rafiki zao kwamba wao wamo katika uwongofu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na kwa hakika, Mashetani wanawazuia hawa wanaoupa mgongo utajo wa Allah Mtukufu wasifuate njia ya haki, wanawapambia upotevu na wanawafanya wachukie Kumuamini Allah Mtukufu na kufanya matendo ya utiifu Kwake. Na wanadhani hawa wenye kupa mgongo, kutokana na vile Mashetani wanavyowapambia upotevu walionao, wanadhani kuwa wao wako kwenye haki na uongofu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Az-Zukhruf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net