Az-Zukhruf 43:38
الزخرفحَتَّىٰٓ إِذَا جَآءَنَا قَالَ يَـٰلَيْتَ بَيْنِى وَبَيْنَكَ بُعْدَ ٱلْمَشْرِقَيْنِ فَبِئْسَ ٱلْقَرِينُ
Hata atakapotujia atasema: 'Laiti ungelikuweko baina yangu na wewe kama umbali baina ya mashariki na magharibi. Rafiki mwovu mno wewe!'
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hata atakapo tujia atasema: Laiti ungeli kuwako baina yangu na wewe kama umbali baina ya mashariki na magharibi. Rafiki mwovu mno wewe! [38]
[38] Hata yule aliye jipa upofu na Qur'ani atapo fika kwa Mwenyezi Mungu Siku ya Kiyama, na akaona matokeo ya kule kujitia kwake upofu, atamwambia rafiki yake kwa majuto: Laiti wewe nami tungeli kuwa mbali mbali duniani umbali wa mashariki na magharibi! Ama wewe ulikuwa sahibu muovu mno kwangu, mpaka umekuja nitumbukize katika shimo la Motoni!
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Mpaka pale atakapotujia yule aliyeupa mgongo utajo wa Allah Mtukufu pamoja na yule mwenzake Shetani, ili kuhesabiwa na kulipwa, atasema yule mwenye kupa mgongo kumwambia mwenzake, «Natamani lau baina yangu mimi na wewe pana umbali wa baina ya Mashariki na Magharibi, kwani rafiki mbaya zaidi kwangu ni wewe kwa kuwa umenipoteza».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net