Az-Zukhruf 43:39
الزخرفوَلَن يَنفَعَكُمُ ٱلْيَوْمَ إِذ ظَّلَمْتُمْ أَنَّكُمْ فِى ٱلْعَذَابِ مُشْتَرِكُونَ
Na kwa kuwa mlidhulumu, haitakufaeni kitu leo kwamba nyinyi mnashirikiana katika adhabu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na kwa kuwa mlidhulumu, haitakufaeni kitu leo kwamba nyinyi mnashirikiana katika adhabu. [39]
[39] Na hapo wataambiwa kwa kuwahizi: Leo hamtapunguziwa adhabu, kwani mmejidhulumu wenyewe kwa ukafiri wenu, kwa sababu mlishirikiana na mashetani wenu. Kwani kila mmoja anateseka kwa adhabu ya kumtosha mwenyewe.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Haitawafaa kitu leo, enyi mlioupa mgongo utajo wa Allah Mtukufu, kwa kushirikisha kwenu duniani, na kwamba mtashirikiana na wenzenu (wa Kishetani) katika adhabu. Basi kila mmoja ana fungu lake kamili la adhabu kama mlivyoshirikiana katika ukanushaji.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net