Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 43 · Aya ya 40

Az-Zukhruf 43:40

الزخرف

أَفَأَنتَ تُسْمِعُ ٱلصُّمَّ أَوْ تَهْدِى ٱلْعُمْىَ وَمَن كَانَ فِى ضَلَـٰلٍ مُّبِينٍ

Maana

Je, unaweza kuwasikilizisha viziwi, au unaweza kuwaongoa vipofu na waliomo katika upotovu ulio wazi?

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Je! Unaweza kuwasikilizisha viziwi, au unaweza kuwaongoa vipofu na waliomo katika upotofu ulio wazi? [40]

[40] Je! Unaweza kumwongoa aliye pita mipaka katika upotovu? Je! Unaweza kumfanya asikie aliye kiziwi hasikii la kweli, kipofu hazingatii, na ambaye katika ujuzi wa Mwenyezi Mungu atakufa katika upotovu? Huwezi hayo! Kwa sababu hao wamekwisha thibiti katika ukafiri wao, basi hawanafiiki kwa wanayo yasikia, wala wanayo yaona.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Kwani wewe, ewe mtume, unamsikilizisha yule ambaye Allah Mtukufu Amemfanya kiziwi akawa haisikii haki, au unamuongoza kwenye njia ya uongofu yule ambaye Allah Mtukufu Ameupofusha moyo wake akawa haioni haki, au unamuongoza yule aliyepotoka waziwazi akawa kando na haki? Hayo si yako. Lako wewe ni kufikisha ujumbe, na si juu yako kuwafanya waongoke, lakini Allah Mtukufu Anamuongoza Anayemtaka na Anampoteza Anayemtaka.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Az-Zukhruf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net