Az-Zukhruf 43:41
الزخرففَإِمَّا نَذْهَبَنَّ بِكَ فَإِنَّا مِنْهُم مُّنتَقِمُونَ
Na hata tukikuondoa, Sisi tutalipiza kisasi chetu kwao.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na hata tukikuondoa, Sisi tutalipiza kisasi chetu kwao. [41]
[41] Basi tukikushika tukakufisha kabla hatuja kuonyesha adhabu yao, na kifua chako kikatua kwa hayo, na pia vifua vya Waumini, alaa kulli hali, Sisi bila ya shaka tutawaadhibu duniani na Akhera.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na iwapo tutakufisha, ewe Mtume, kabla hujanusuriwa juu ya wakanushaji wa watu wako, basi sisi ni wenye kuwalipiza wao kwa kuwaadhibu huko Akhera.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net