Az-Zukhruf 43:42
الزخرفأَوْ نُرِيَنَّكَ ٱلَّذِى وَعَدْنَـٰهُمْ فَإِنَّا عَلَيْهِم مُّقْتَدِرُونَ
Au tutakuonyesha tuliyowaahidi. Nasi bila ya shaka tuna uweza juu yao.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Au tutakuonyesha tulio waahidi. Nasi bila ya shaka tuna uweza juu yao. [42]
[42] Au unataka tukuonyeshe adhabu tuliyo waahidi kabla ya kufa kwako, tutakuonyesha, kwani Sisi tunawaweza hao kwa uweza wetu na nguvu zetu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Au tutakuonyesha lile tulilowaahidi la adhabu yenye kuwashukia, kama ilivyokuwa siku ya (Badr), kwani sisi tuna uwezo juu yao, tutakupa ushindi juu yao na tutawafedhehi kwa mkono wako na kwa mikono ya wenye kukuamini.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net