Fussilat 41:45
فصلتوَلَقَدْ ءَاتَيْنَا مُوسَى ٱلْكِتَـٰبَ فَٱخْتُلِفَ فِيهِ ۗ وَلَوْلَا كَلِمَةٌ سَبَقَتْ مِن رَّبِّكَ لَقُضِىَ بَيْنَهُمْ ۚ وَإِنَّهُمْ لَفِى شَكٍّ مِّنْهُ مُرِيبٍ
Na hakika tulimpa Musa Kitabu, lakini pakatokea tofauti juu yake. Na lau kuwa halikwisha tangulia neno la Mola wako Mlezi, wangelihukumiwa. Na hakika wao wamo katika shaka yenye kuwatia wasiwasi juu yake.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na hakika tulimpa Musa Kitabu, lakini pakatokea khitilafu kati yake. Na lau kuwa halikwisha tangulia neno la Mola wako Mlezi wangeli hukumiwa. Na hakika wao wamo katika shaka yenye kuwatia wasiwasi. [45]
[45] Ninaapa: Kwa hakika tulimpa Musa Taurati, na watu wake wakakhitalifiana kwayo. Na lau ingeli kuwa hukumu ya Mola wako Mlezi haikuakhirishwa, ewe Muhammad, mpaka muda maalumu kwake, basi hapana shaka pange amuliwa hukumu baina yako na hao kwa kuwang'olea mbali wanao kanusha. Na hakika makafiri katika kaumu yako wamo katika shaka na Qur'ani, na hiyo inawatia dhiki na wasiwasi.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hakika tulimpelekea Mûsã Taurati kama tulivyokuletea wewe, (ewe Mtume), Qur’ani, wakatafautiana watu wake kuhusu hiyo: katika wao kuna aliyeamini na katika wao kuna aliyekanusha. Na lau si neno (la ahadi) lililotangulia kutoka kwa Mola wako la kuwacheleweshea watu wako adhabu, uamuzi baina yao ungetolewa wa kuwaangamiza makafiri papo hapo. Na kwa hakika washirikina wana shaka nayo sana Qur’ani.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net