Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 41 · Aya ya 46

Fussilat 41:46

فصلت

مَّنْ عَمِلَ صَـٰلِحًا فَلِنَفْسِهِۦ ۖ وَمَنْ أَسَآءَ فَعَلَيْهَا ۗ وَمَا رَبُّكَ بِظَلَّـٰمٍ لِّلْعَبِيدِ

Maana

Anayetenda mema, basi anajitendea mwenyewe nafsi yake. Na mwenye kutenda uovu, basi ni juu ya nafsi yake vile vile; wala Mola wako Mlezi si mwenye kuwadhulumu waja.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Anaye tenda mema basi anajitendea mwenyewe nafsi yake, na mwenye kutenda uovu basi ni juu ya nafsi yake vile vile; wala Mola wako Mlezi si mwenye kuwadhulumu waja. [46]

[46] Mwenye kutenda vitendo vyema ujira wake ataupata mwenyewe, na mwenye kutenda uovu madhambi yake yatakuwa juu yake. Na Mola wako Mlezi si mwenye kuwadhulumu waja wake, hata amtese mtu kwa dhambi za mwengine.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Mwenye kufanya mema, akamtii Allah Mtukufu na Mtume Wake, atajipatia mwenyewe thawabu za matendo yake. Na mwenye kumuasi Allah Mtukufu na Mtume Wake, atajionea mwenyewe dhambi za matendo yake. Na Mola wako si Mwenye kuwadhulumu waja kwa kuwapunguzia japo thawabu ya jema moja au kuwaongezea japo dhambi ya ovu moja.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Fussilat

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net