Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 41 · Aya ya 47

Fussilat 41:47

فصلت

إِلَيْهِ يُرَدُّ عِلْمُ ٱلسَّاعَةِ ۚ وَمَا تَخْرُجُ مِن ثَمَرَٰتٍ مِّنْ أَكْمَامِهَا وَمَا تَحْمِلُ مِنْ أُنثَىٰ وَلَا تَضَعُ إِلَّا بِعِلْمِهِۦ ۚ وَيَوْمَ يُنَادِيهِمْ أَيْنَ شُرَكَآءِى قَالُوٓا۟ ءَاذَنَّـٰكَ مَا مِنَّا مِن شَهِيدٍ

Maana

Ujuzi wa kuijua Saa ya Kiyama unarudishwa kwake tu Mwenyezi Mungu. Na matunda hayatoki katika mafumba yake, wala cha kike hakichukui mimba, wala hakizai, ila kwa kujua kwake. Na siku atakayowaita, akawaambia: 'Wako wapi washirika wangu?' Hapo watasema: 'Tunakiri kwako ya kwamba hapana miongoni mwetu anayeshuhudia hayo.'

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

UJUZI wa kuijua Saa ya Kiyama unarudishwa kwake tu Mwenyezi Mungu. Na matunda hayatoki katika mafumba yake, wala mwanamke hachukui mimba, wala hazai, ila kwa kujua kwake. Na siku atakayo waita, akawaambia: Wako wapi washirika wangu? Hapo watasema: Tunakiri kwako ya kwamba hapana miongoni mwetu anaye shuhudia hayo. [47]

[47] Kwa Mwenyezi Mungu peke yake ndio unarejea ujuzi wa kusimama Saa ya Kiyama. Matunda hayatoki kwenye vifuniko vyake, wala mwanamke hachukui mimba wala hazai ila awe Yeye anajua. Na kumbuka siku ambayo Mwenyezi Mungu atawaita washirikina, kwa kuwakebehi, awaambie: Wako wapi hao washirika wangu mlio kuwa mkiwaomba badala yangu? Watasema kwa kutaadhari: Ewe Mwenyezi Mungu! Tunakujuvya kuwa sisi hatuna wa kushuhudia kuwa wewe una mshirika yeyote.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Kwa Allah Mtukufu Aliyetukuka, Peke Yake, Asiye na mshirika, Ndiko kunakorudishwa ujuzi wa kipindi cha kusimama Kiyama, kwani hakuna yoyote anayejua kipindi hicho isipokuwa Yeye. Na hayatoki matunda kwenye vifuko vyake (mitini), na hakuna kiumbe chochote cha kike kinachoshika mimba wala kinachojifungua mimba yake isipokuwa kinajulikana na Allah Mtukufu. Hakuna chochote kinachofichika kwake kuhusu hilo. Na siku ambayo Allah Mtukufu Aliyetukuka Atawaita washirikina Siku ya Kiyama kwa kuwakaripia na kuonyesha urongo wao, Awaambie, Wako wapi washirika wangu ambao mlikuwa mkiwashirikisha katika ibada yangu? Hapo watasema, «Tunakujulisha sasa kuwa hatuna yoyote atakayeshuhudia Leo kuwa wewe una mshirika».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Fussilat

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net