Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 41 · Aya ya 44

Fussilat 41:44

فصلت

وَلَوْ جَعَلْنَـٰهُ قُرْءَانًا أَعْجَمِيًّا لَّقَالُوا۟ لَوْلَا فُصِّلَتْ ءَايَـٰتُهُۥٓ ۖ ءَا۬عْجَمِىٌّ وَعَرَبِىٌّ ۗ قُلْ هُوَ لِلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ هُدًى وَشِفَآءٌ ۖ وَٱلَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ فِىٓ ءَاذَانِهِمْ وَقْرٌ وَهُوَ عَلَيْهِمْ عَمًى ۚ أُو۟لَـٰٓئِكَ يُنَادَوْنَ مِن مَّكَانٍۭ بَعِيدٍ

Maana

Na lau tungeliifanya Qur-ani kwa lugha ya kigeni, wangelisema: Kwa nini Aya zake hazikupambanuliwa? Yawaje lugha ya kigeni na Mtume Mwaarabu? Sema: Hii Qur-ani ni uongofu na ponya kwa wenye kuamini. Na wale wasioamini umo uziwi katika masikio yao, nayo kwao imezibwa hawaioni. Hao wanaitwa nao wako pahala mbali.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na lau tungeli ifanya Qur'ani kwa lugha ya kigeni wangeli sema: Kwanini Aya zake haziku pambanuliwa? Yawaje lugha ya kigeni na Mtume Mwaarabu? Sema: Hii Qur'ani ni uwongofu na poza kwa wenye kuamini. Na wasio amini umo uziwi katika masikio yao, nayo kwao imezibwa hawaioni. Hao wanaitwa nao wako pahala mbali. [44]

[44] Na lau tungeli ifanya Qur'ani kwa lugha ya kigeni, kama walivyo pendekeza baadhi ya hao wanao kera, basi bila ya shaka wangeli sema: Lau zingeli bainishwa Aya zake kwa ulimi tunao ufahamu! Kitabu hichi cha lugha ya kigeni, na huyu mkhubiri wake ni Mwaarabu! Yawaje haya? Ewe Mtume! Waambie: Hii Qur'ani ni hivyo hivyo kama walivyo teremshiwa Waumini, si wengineo, kuwa ni Uwongofu na Poza kwa Waumini; kiwaokoe na ubabaishi, na kiwaponyeshe na shaka shaka. Na wasio amini wamekuwa kama katika masikio yao pana kizuizi, uziwi, nayo hii Qur'ani kwao wao ni upofu, hawaoni chochote ndani yake ila fitna tu. Hao makafiri ni kama wanao itwa waiamini kwa umbali kabisa. Hawausikii wito huo.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na lau tungeifanya hii Qur’ani tuliyokuteremshia, (ewe Mtume), ni kwa lugha isiyokuwa ya Kiarabu, washirikina wangesema, «Je, si zifafanuliwe aya zake tupate kuzifahamu na kuzijua? Ni vipi hii Qur’ani ni kwa lugha isiyokuwa ya Kiarabu na hali lugha ya huyu aliyeteremshiwa ni ya Kiarabu? Hili haliwi!» Waambie, ewe Mtume, «Hii Qur’ani, kwa wale waliomuamini Allah Mtukufu na Mtume Wake, ni uongofu kutoka kwenye upotevu na ni ponyesho la yaliyomo vifuani ya shaka na magonjwa. Na wale wasioiamini Qur’ani kuna uziwi ndani ya masikio yao unaowafanya wasiisikie na wasiizingatie; na nyoyo zao zina upofu wa kutoongoka na Qur’ani» Basi washirikina hao ni kama yule anayeitwa ambaye yuko mbali, hamsikii mwenye kumuita wala hamuitikii.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Fussilat

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net