Fussilat 41:37
فصلتوَمِنْ ءَايَـٰتِهِ ٱلَّيْلُ وَٱلنَّهَارُ وَٱلشَّمْسُ وَٱلْقَمَرُ ۚ لَا تَسْجُدُوا۟ لِلشَّمْسِ وَلَا لِلْقَمَرِ وَٱسْجُدُوا۟ لِلَّهِ ٱلَّذِى خَلَقَهُنَّ إِن كُنتُمْ إِيَّاهُ تَعْبُدُونَ
Na katika Ishara zake ni usiku na mchana, na jua na mwezi. Basi msilisujudie jua wala mwezi, bali msujudieni Mwenyezi Mungu aliyeviumba, ikiwa nyinyi mnamuabudu Yeye tu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na katika Ishara zake ni usiku na mchana, na jua na mwezi. Basi msilisujudie jua wala mwezi, bali msujudieni Mwenyezi Mungu aliye viumba, ikiwa nyinyi mnamuabudu Yeye tu. [37]
[37] Na katika dalili za uweza wake Mwenyezi Mungu Mtukufu ni huu usiku na mchana, na jua na mwezi. Msilisujudie jua wala mwezi, kwani hivyo ni katika Ishara zake tu. Bali msujudieni Yeye Mwenyezi Mungu peke yake, aliye umba jua, na mwezi, na usiku, na mchana, ikiwa nyinyi kweli mnamuabudu Yeye peke yake.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na miongoni mwa hoja za Allah Mtukufu kwa viumbe Vyake, dalili za upweke Wake na ukamilifu wa uwezo Wake, ni kutafautiana mchana na usiku na kufuatana (kila mojawapo kuufuata kingine) na kutafautiana jua na mwezi na kufuatana, vyote hivyo viko chini ya uendeshaji Wake na utendeshaji nguvu Wake. Msilisujudie jua wala mwezi, kwani hivyo viwili vinaendeshwa na vimeumbwa; na msujudieni Allah Mtukufu Aliyeviumba, iwapo nyinyi kweli mnafuata amri Yake, mnasikia na mnamtii Yeye, basi muabuduni Yeye Peke Yake Asiye na mshirika.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net