Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 41 · Aya ya 38

Fussilat 41:38

فصلت

فَإِنِ ٱسْتَكْبَرُوا۟ فَٱلَّذِينَ عِندَ رَبِّكَ يُسَبِّحُونَ لَهُۥ بِٱلَّيْلِ وَٱلنَّهَارِ وَهُمْ لَا يَسْـَٔمُونَ ۩

Maana

Na ikiwa watajivuna, basi hao walioko kwa Mola wako Mlezi wanamtakasa Yeye usiku na mchana, na wao hawachoki.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na ikiwa watajivuna, basi hao walioko kwa Mola wako Mlezi wanamtakasa Yeye usiku na mchana, na wao hawachoki. [38]

[38] Ikiwa washirikina watajiona wakubwa hawafai kufuata amri yako, basi wewe usiudhike. Kwani hao walio kwa Mola wako Mlezi kwenye utakatifu wake, nao ni Malaika, wanamtakasa Yeye na kila upungufu katika kila wakati, usiku na mchana, wakimsafia ibada Yeye tu, wala hawachoki kumsabihi.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na wakifanya kiburi washirikina hawa kwa kukataa kumsujudia Allah Mtukufu, basi Malaika waliyoko kwa Mola wako hawafanyi kiburi cha kukataa hilo, bali wanamsujudia Yeye na wanamtakasa na kila upungufu, usiku na mchana, na wao hawapumziki na hilo wala hawachoki.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Fussilat

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net