Fussilat 41:39
فصلتوَمِنْ ءَايَـٰتِهِۦٓ أَنَّكَ تَرَى ٱلْأَرْضَ خَـٰشِعَةً فَإِذَآ أَنزَلْنَا عَلَيْهَا ٱلْمَآءَ ٱهْتَزَّتْ وَرَبَتْ ۚ إِنَّ ٱلَّذِىٓ أَحْيَاهَا لَمُحْىِ ٱلْمَوْتَىٰٓ ۚ إِنَّهُۥ عَلَىٰ كُلِّ شَىْءٍ قَدِيرٌ
Na katika Ishara zake ni kwamba unaiona ardhi nyonge, lakini tunapoiteremshia maji, mara unaiona inataharaki na kuumuka. Bila ya shaka yule aliyeihuisha ardhi ndiye atakayehuisha wafu. Hakika Yeye ni Muweza mno wa kila kitu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na katika Ishara zake ni kwamba unaiona ardhi nyonge, lakini tunapo iteremshia maji mara unaiona inataharaki na kuumuka. Bila ya shaka aliye ihuisha ardhi ndiye atakaye huisha wafu. Hakika Yeye ni Muweza wa kila kitu. [39]
[39] Na katika dalili za uweza wake, Mtukufu, ni kwamba unaona, wewe unaye weza kuona, ardhi kavu. Tukiiteremshia maji inatikisika kwa mimea, na inaumuka na kuja juu. Hakika huyo aliye ihuisha ardhi iliyo kwisha kufa ndiye aliye elekea kuhuisha wafu katika hayawani. Yeye ni mtimilivu wa uweza juu ya kila kitu. Aya hii inabainisha kwamba mawadi za mbolea ambazo ni chumvi chumvi zisio na uhai, pindi zipatapo maji ya mvua, huyayuka, na kwa hivyo husahilika kufikilia kwenye mbegu za mimea na mizizi yake. Hapo hugeuka kuingia katika khalaya (Cells) na mifumo na viungo vilio hai. Na kwa hivyo vinaonekana kuwa ni hai. Na ukubwa wake hukua na kuzidi kwa kuingiana na kukuzwa na mimea.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na miongoni mwa alama za upweke wa Allah Mtukufu na uwezo Wake ni kuwa unaiona ardhi ikiwa kavu haina mimea, na tunapoiteremshia mvua, uhai unatambaa ndani yake na inasukikasukika kwa mimea, na inavimba na kunyanyuka. Hakika Yule aliyeihuisha ardhi hii baada ya ukavu wake ni Muweza wa kuwahuisha viumbe baada ya kufa kwao. Hakika Yeye juu ya kila jambo ni Muweza. Na kama usivyoelemewa uwezo Wake kuhuisha ardhi baada ya kufa kwake, hivyo hivyo uwezo Wake hauelemewi kuwahuisha waliokufa.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net