Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 41 · Aya ya 40

Fussilat 41:40

فصلت

إِنَّ ٱلَّذِينَ يُلْحِدُونَ فِىٓ ءَايَـٰتِنَا لَا يَخْفَوْنَ عَلَيْنَآ ۗ أَفَمَن يُلْقَىٰ فِى ٱلنَّارِ خَيْرٌ أَم مَّن يَأْتِىٓ ءَامِنًا يَوْمَ ٱلْقِيَـٰمَةِ ۚ ٱعْمَلُوا۟ مَا شِئْتُمْ ۖ إِنَّهُۥ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ

Maana

Hakika wale wanaopindukia mipaka katika Ishara zetu, hawafichikani kwetu. Je, atakayetupwa Motoni ni bora au atakayekuja kwa amani Siku ya Kiyama? Tendeni mpendavyo, kwa hakika Yeye anayaona vyema mnayoyatenda.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Hakika wale wanao upotoa ukweli uliomo katika Ishara zetu hawatufichikii Sisi. Je! Atakaye tupwa Motoni ni bora au atakaye kuja kwa amani Siku ya Kiyama? Tendeni mpendavyo, kwa hakika Yeye anayaona mnayo yatenda. [40]

[40] Hakika hao wanao iacha Njia iliyo sawa kwa mintarafu ya Ishara zetu na wakaitupilia mbali kwa kuikadhibisha, mambo yao hayatupotei Sisi wala hayo wanayo yakusudia. Nasi tutawalipa kama wanavyo stahiki. Kwani anaye tupwa katika Moto ni bora au yule anaye kuja naye hali katulia Siku ya Kiyama kwa kuokoka kwake na kila ovu? Kabisa hao hawalingani. Waambie kwa kuwaahidi: Fanyeni mtakavyo. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuzunguka kila kitu kwa jicho lake, naye atamlipa kila mmoja kwa a'mali yake.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hakika wale wanaopotoka na haki wakaikanusha Qur’ani na wakaipotoa, hawafichiki kwetu, bali sisi tunawaona wao. Je, huyu mwenye kuzipotosha aya za Allah Mtukufu atakayetiwa Motoni ndiye bora au ni yule atakayekuja Siku ya Kiyama hali ya kuwa amesalimika na adhabu ya Allah Mtukufu na kustahiki malipo mema Yake kwa kumuamini na kuzisadiki aya Zake? Fanyeni, enyi wapotofu, mnalolitaka, kwani Allah Mtukufu, Aliyetukuka, Anayaona matendo yenu, hakuna kinachofichika Kwake, na Atawalipa kwa hayo. Hapa pana onyo na tahadharisho kwao.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Fussilat

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net