Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 41 · Aya ya 36

Fussilat 41:36

فصلت

وَإِمَّا يَنزَغَنَّكَ مِنَ ٱلشَّيْطَـٰنِ نَزْغٌ فَٱسْتَعِذْ بِٱللَّهِ ۖ إِنَّهُۥ هُوَ ٱلسَّمِيعُ ٱلْعَلِيمُ

Maana

Na Shetani akikuchochea kwa uchochezi, wewe jikinge kwa Mwenyezi Mungu. Hakika Yeye ni Mwenye kusikia, ajuaye zaidi.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na Shet'ani akikuchochea kwa uchochezi wewe jikinge kwa Mwenyezi Mungu. Hakika Yeye ni Mwenye kusikia, Mwenye kujua. [36]

[36] Na akitokea Shetani akakutia wasiwasi kukuachisha hayo uliyo amrishwa, ewe unaye semezwa, basi jilinde naye kwa Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu kusikia kwake na kujua kwake kumezunguka kila kitu. Na Yeye atakulinda naye.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na Shetani anapotia ndani ya nafsi yako ushawishi wa mawazo ya kukufanya umlipe baya kwa ubaya, basi omba himaya ya Allah Mtukufu na ushikamane naye. Kwani Allah Mtukufu ni Mwenye kusikia sana maombi yako ya kujilinda Kwake, ni Mwenye kuyajua sana mambo ya viumbe Vyake vyote.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Fussilat

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net