Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 41 · Aya ya 35

Fussilat 41:35

فصلت

وَمَا يُلَقَّىٰهَآ إِلَّا ٱلَّذِينَ صَبَرُوا۟ وَمَا يُلَقَّىٰهَآ إِلَّا ذُو حَظٍّ عَظِيمٍ

Maana

Lakini hawapewi wema huu ila wanaosubiri, wala hawapewi ila wenye bahati kubwa.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Lakini hawapewi wema huu ila wanao subiri, wala hawapewi ila wenye bahati kubwa. [35]

[35] Na hawaruzukiwi tabia hii, ya kulipa wema kwa uovu, ila wale wenye khulka ya kusubiri, na hawaruzukiwi hayo ila wenye fungu kubwa la tabia ya wema na ukamilifu wa nafsi.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na hawaafikiwi kwenye mambo haya yanayosifika vyema isipokuwa wale wanaojisubirisha juu ya mambo ambayo nafsi zao zinayachukia, na wakajilazimisha kwa yale Anayoyapenda Allah Mtukufu. Na haafikiwi hayo isipokuwa mwenye fungu kubwa la hali njema ya duniani na Akhera.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Fussilat

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net