Fussilat 41:34
فصلتوَلَا تَسْتَوِى ٱلْحَسَنَةُ وَلَا ٱلسَّيِّئَةُ ۚ ٱدْفَعْ بِٱلَّتِى هِىَ أَحْسَنُ فَإِذَا ٱلَّذِى بَيْنَكَ وَبَيْنَهُۥ عَدَٰوَةٌ كَأَنَّهُۥ وَلِىٌّ حَمِيمٌ
Mema na maovu hayalingani. Pinga uovu kwa lililo jema zaidi. Hapo yule ambaye baina yako naye pana uadui atakuwa kama rafiki jamaa wa kukuonea uchungu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Mema na maovu hayalingani. Pinga uovu kwa lilio jema zaidi. Hapo yule ambaye baina yako naye pana uadui atakuwa kama rafiki jamaa wa kukuonea uchungu. [34]
[34] Haziwezi kuwa sawa tabia njema na tabia mbovu. Pinga uovu ukikujia kutokana na adui kwa tabia iliyo bora kuliko yake. Hapo matokeo yake ni huyo ambaye uliye kuwa na uadui naye atakuja kuwa kama mwenzio wa kukunusuru mwenye moyo safi.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na halilingani jema la waliomuamini Allah Mtukufu, wakasimama imara kwenye Sheria Yake, wakawafanyia wema viumbe Vyake (hilo halilingani) na baya la waliomkanusha Yeye, wakaenda kinyume na amri Yake na wakawafanyia ubaya viumbe Vyake. Mzuiye, ewe Mtume, kwa msamaha wako, upole wako na hisani yako yule anayekufanyia ubaya, kwa kumfanyia wema. Hivyo basi yule aliyekutendea ubaya ambaye baina yako na yeye kuna uadui atakuwa kana kwamba ni mtu aliye jamaa yako wa karibu na mwenye huruma na wewe.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net