Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 4 · Aya ya 97

An-Nisaa 4:97

النساء

إِنَّ ٱلَّذِينَ تَوَفَّىٰهُمُ ٱلْمَلَـٰٓئِكَةُ ظَالِمِىٓ أَنفُسِهِمْ قَالُوا۟ فِيمَ كُنتُمْ ۖ قَالُوا۟ كُنَّا مُسْتَضْعَفِينَ فِى ٱلْأَرْضِ ۚ قَالُوٓا۟ أَلَمْ تَكُنْ أَرْضُ ٱللَّهِ وَٰسِعَةً فَتُهَاجِرُوا۟ فِيهَا ۚ فَأُو۟لَـٰٓئِكَ مَأْوَىٰهُمْ جَهَنَّمُ ۖ وَسَآءَتْ مَصِيرًا

Maana

Hakika, wale ambao Malaika wanawafisha hali ya kuwa wamezidhulumu nafsi zao, watawaambia: 'Mlikuwa katika nini?' Watasema: 'Tulikuwa tumefanywa kuwa wanyoge katika ardhi.' Watawaambia: 'Kwani ardhi ya Mwenyezi Mungu haikuwa na wasaa, mkahamie humo?' Basi hao makazi yao ni Jahannam, nayo ni marejeo mabaya kabisa.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Hakika Malaika watawaambia wale ambao wamewafisha nao wamejidhulumu nafsi zao: Mlikuwa vipi? Watasema: Tulikuwa tunaonewa. Watawaambia: Kwani ardhi ya Mwenyezi Mungu haikuwa na wasaa wa kuhamia humo? Basi hao makaazi yao ni Jahannamu, nayo ni marejeo mabaya kabisa. [97]

[97] Na hakika ni waajibu wa Muislamu kuhamia kwenye dola ya Kiislamu asiishi katika udhalili. Malaika watawauliza wakisha kufa: Mlikuwaje hata mkaridhia maisha ya unyonge na kudharauliwa? Na wao watajibu: Tulikuwa wanyonge katika nchi hiyo tukionewa. Malaika watawaambia: Kwani ardhi ya Mwenyezi Mungu haikuwa kunjufu ina wasaa, mkaweza kuhama badala ya kuishi katika uonevu? Watu hao wanao kubali uonevu, na wao wanaweza kuondoka, makao yao yatakuwa ni Jahannamu. Na hayo ni mashukio maovu kabisa. Basi Muislamu haimfalii kuishi katika udhalili, bali aishi na utukufu wake na hishima yake.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hakika wale ambao Malaika waliwafisha na wao wako katika hali ya kujidhulumu wenyewe kwa kukaa katika nchi ya ukafiri na kuacha kuhama, Malaika watawaambia kwa njia ya kuwalaumu, «Mlikuwa katika nini kuhusu mambo ya Dini yenu?» watasema, «Tulikuwa wanyonge nchini kwetu, tumelemewa kuweza kujiepushia dhuluma na maonevu.» Malaika watawaambia kwa njia ya kuwalaumu, «Kwani ardhi ya Allah Mtukufu haikuwa kunjufu mkatoka kwenye ardhi yenu mkaenda ardhi nyingine ambapo mtapata amani na Dini yenu?» Basi hao makao yao ni Moto. Na haya ni makao mabaya ya mtu kuishilia.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Nisaa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net