Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 4 · Aya ya 98

An-Nisaa 4:98

النساء

إِلَّا ٱلْمُسْتَضْعَفِينَ مِنَ ٱلرِّجَالِ وَٱلنِّسَآءِ وَٱلْوِلْدَٰنِ لَا يَسْتَطِيعُونَ حِيلَةً وَلَا يَهْتَدُونَ سَبِيلًا

Maana

Isipokuwa wale waliodhoofishwa miongoni mwa wanaume na wanawake na watoto wasioweza hila wala hawawezi kufuata sawasawa njia ya kuhama.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Isipo kuwa wale walio kuwa wanyonge miongoni mwa wanaume na wanawake na watoto wasio na uweza wa hila ya kuongoza njia ya kuhama. [98]

[98] Juu ya hivyo wanasameheka na adhabu hii wale wasio weza kusafiri miongoni mwa wanaume, na wanawake, na watoto, wasio na nguvu, na hawana hila, wala hawakupata njia ya kutoka.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Wataepushwa na mwisho huo wakongwe wanaume na wanawake na watoto ambao hawawezi kujiondolea udhalimu na uonevu na hawajui njia yoyote ya kuwaokoa wao na mateso.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Nisaa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net