Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 4 · Aya ya 99

An-Nisaa 4:99

النساء

فَأُو۟لَـٰٓئِكَ عَسَى ٱللَّهُ أَن يَعْفُوَ عَنْهُمْ ۚ وَكَانَ ٱللَّهُ عَفُوًّا غَفُورًا

Maana

Basi hao, huenda Mwenyezi Mungu akawasamehe. Na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kusamehe, Mwingi wa kufuta dhambi.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Basi hao huenda Mwenyezi Mungu akawasamehe. Na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kusamehe, Mwingi wa maghfira [99]

[99] Na hao wanatarajiwa kupata msamaha wa Mwenyezi Mungu. Na ni shani yake Mwenyezi Mungu kusamehe na kughufiria.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Wanyonge hawa ndio wanaotarajiwa kupata msamaha kutoka kwa Allah Mtukufu, kwa kuwa Yeye Anaujua uhakika wa mambo yao. Na Allah Mtukufu ni Mwingi wa msamaha, Anawasamehe makosa yao na Anawafinikia na kuwasitiria.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Nisaa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net