An-Nisaa 4:100
النساءوَمَن يُهَاجِرْ فِى سَبِيلِ ٱللَّهِ يَجِدْ فِى ٱلْأَرْضِ مُرَٰغَمًا كَثِيرًا وَسَعَةً ۚ وَمَن يَخْرُجْ مِنۢ بَيْتِهِۦ مُهَاجِرًا إِلَى ٱللَّهِ وَرَسُولِهِۦ ثُمَّ يُدْرِكْهُ ٱلْمَوْتُ فَقَدْ وَقَعَ أَجْرُهُۥ عَلَى ٱللَّهِ ۗ وَكَانَ ٱللَّهُ غَفُورًا رَّحِيمًا
Na mwenye kuhama katika Njia ya Mwenyezi Mungu, atapata pengi duniani pa kukimbilia, na atapata wasaa. Na mwenye kutoka katika nyumba yake akihamia kwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake, kisha yakamfika mauti, basi hakika umekwishawajibika ujira wake kwa Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kufuta dhambi, Mwenye kurehemu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na mwenye kuhama katika Njia ya Mwenyezi Mungu atapata pengi duniani pa kukimbilia, na atapata wasaa. Na anaye toka nyumbani kwake kuhama kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake, kisha yakamfika mauti njiani basi umethibiti ujira wake kwa Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye maghfira na Mwenye kurehemu. [100]
[100] Anaye hama kutafuta njia za kuiwania Haki na kuiunga mkono, atakuta duniani kwingi endako ambako maadui wa Haki wanahizika. Na atapata wasaa wa uhuru, na makao ya hishima,na thawabu, na ujira mkubwa. Aliye toka kwake kuhamia dola ya hishima, ambayo ndiyo dola ya Mwenyezi Mungu na Mtumewe, kisha yakamdiriki mauti kabla hajafika endako, basi ujira wake umethibiti. Mwenyezi Mungu amemkirimu kwa kujiwajibishia kumlipa ujira wake, na kumghufiria na kumrehemu. Ni shani yake kughufiria na kurehemu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na yoyote mwenye kutoka kwenye ardhi ya ushirikina kwenda kwenye ardhi ya Uislamu kwa ajili ya kukimbia na dini Yake, akitaraji fadhila za Mola wake na akikusudia kuinusuru dini Yake, atapata katika ardhi mahali pa kuelekea ambapo ataneemeka, pawe ni sababu ya yeye kupata nguvu na maadui zake kuwa wanyonge, pamoja na kupata ukunjufu wa riziki na maisha. Na yoyote mwenye kutoka nyumbani kwake kwa lengo la kuinusuru dini ya Allah Mtukufu na Mtume Wake, rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukiye na kulitukuza neno la Allah Mtukufu kisha akapatikana na kifo kabla ya kufikia lengo lake, basi malipo ya kitendo chake yameshathibiti kwa Allah Mtukufu, kwa fadhila Zake na wema Wake. Na Allah Mtukufu ni Mwingi wa msamaha, ni Mwingi wa huruma kwa waja Wake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net