An-Nisaa 4:101
النساءوَإِذَا ضَرَبْتُمْ فِى ٱلْأَرْضِ فَلَيْسَ عَلَيْكُمْ جُنَاحٌ أَن تَقْصُرُوا۟ مِنَ ٱلصَّلَوٰةِ إِنْ خِفْتُمْ أَن يَفْتِنَكُمُ ٱلَّذِينَ كَفَرُوٓا۟ ۚ إِنَّ ٱلْكَـٰفِرِينَ كَانُوا۟ لَكُمْ عَدُوًّا مُّبِينًا
Na mnaposafiri katika nchi, basi hakuna ubaya juu yenu mkifupisha katika Swala, iwapo mnachelea kwamba wale waliokufuru watawajaribu. Hakika, makafiri ni maadui zenu walio wazi.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na mnapo safiri katika nchi si vibaya kwenu kama mkifupisha Swala, iwapo mnachelea wasije wale walio kufuru wakakuleteeni maudhi. Hakika makafiri ni maadui zenu walio wazi wazi. [101]
[101] Swala ni faridha isiyo epukika. Haiachiki Swala kwa ajili ya safari, lakini hana dhambi anaye fupisha Swala safarini. Watokao kwenda safari wakikhofia kuwa makafiri watawaletea ya kuwaudhi, wanaweza kufupisha Swala. Swala za rakaa nne zisaliwe rakaa mbili. Kutahadhari na kuingiliwa na makafiri ni waajibu, kwani wao ni maadui, na uadui wao uwazi.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na mnaposafiri, enyi Waumini, kwenye ardhi ya Allah Mtukufu, hamuna makosa wala dhambi kupunguza Swala, mkiogopa kufanyiwa uadui na makafiri mkiwa kwenye Swala. Safari nyinygi za Waislamu, katika mwanzo wa Uislamu, zilikuwa za kutisha. Na kupunguza Swala ni ruhusa iliyotolewa kwenye safari, katika hali ya amani au vitisho. Hakika makafiri ni wenye kudhihirisha uadui wao kwenu, basi jihadharini nao.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net