An-Nisaa 4:96
النساءدَرَجَـٰتٍ مِّنْهُ وَمَغْفِرَةً وَرَحْمَةً ۚ وَكَانَ ٱللَّهُ غَفُورًا رَّحِيمًا
Hivyo ni vyeo kutoka kwake, na kufutiwa dhambi, na rehema. Na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kufuta dhambi, na Mwenye kurehemu sana.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Ni vyeo hivyo vinavyo toka kwake, na maghfira na rehema. Na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa maghfira na Mwenye kurehemu. [96]
[96] Na cheo hichi walicho khusishwa nacho hao wanao pigana Jihadi ni cheo kikubwa, cha juu, hata imekuwa ni kama cheo cha kutafautisha sana baina yao na wengineo. Na kwa ajili ya cheo hichi watapata maghfira makubwa na rehema kunjufu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Thawabu nyingi hizi ni daraja za juu, katika mabustani ya Pepo, zitokazo kwa Allah Mtukufu, walizopewa waja Wake maalumu wenye kupigana katika njia Yake, na msamaha wa madhambi yao na rehema kunjufu ambayo ndani yake wananeemeshwa. Allah Mtukufu ni Mwingi wa msamaha kwa anayetubia Kwake na kurejea, ni Mwingi wa rehema kwa wenye kumtii, wenye kupigana jihadi katika njia Yake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net