An-Nisaa 4:88
النساءفَمَا لَكُمْ فِى ٱلْمُنَـٰفِقِينَ فِئَتَيْنِ وَٱللَّهُ أَرْكَسَهُم بِمَا كَسَبُوٓا۟ ۚ أَتُرِيدُونَ أَن تَهْدُوا۟ مَنْ أَضَلَّ ٱللَّهُ ۖ وَمَن يُضْلِلِ ٱللَّهُ فَلَن تَجِدَ لَهُۥ سَبِيلًا
Basi mna nini mmekuwa makundi mawili kuhusiana na (habari ya) wanafiki, na ilhali Mwenyezi Mungu amewageuza kwa sababu ya yale waliyoyachuma? Je, mnataka kumwongoa yule ambaye Mwenyezi Mungu amempoteza? Na mwenye kupotezwa na Mwenyezi Mungu, basi wewe hutapata njia yoyote kwa ajili yake.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Mmekuwaje kuwa makundi mawili kwa khabari ya wanaafiki, na hali Mwenyezi Mungu amewageuza kwa sababu ya yale waliyo yachuma? Je! Mnataka kumwona mwongofu ambaye Mwenyezi Mungu amemhukumu kuwa kapotea? Na aliye mhukumu Mwenyezi Mungu kuwa amekwisha potea wewe hutampatia njia. [88]
[88] Haikufaliini, enyi Waumini, kukhitalifiana katika mas-ala yaliyo khusu wanaafiki, ambao wanadhihirisha Uislamu na wanaficha ukafiri. Haikufaliini kukhitalifiana kwa mas-ala yao, kuwa ati wao ni Waumini au makafiri? Wauwawe au waachiliwe? Je, wameelekea kuongoka au hawatarajiwi uwongofu? Fahamu zao zimegeuzwa kwa yaliyo chumwa na vitendo vyao. Shari imekuwa ndio inayo wahukumu, basi usimtarajie kuongoka yule ambaye Mwenyezi Mungu kwa ujuzi wake wa tangu na tangu kesha mkadiria asiongoke. Kwani aliye andikwa katika ujuzi wa Mwenyezi Mungu wa tangu azali kuwa ni mwenye kupotea basi huna njia ya kumwongoa.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Muna nini nyinyi, enyi Waumini, mumetafautiana makundi mawili kuhusu wanafiki: kundi linasema kwamba wapigwe vita na lingine halisemi hivyo? Na hali Allah Mtukufu Amewatia kwenye ukafiri na upotevu kwa sababu ya vitendo vyao. Kwani mnataka kumpa uongofu yule ambaye Allah Mtukufu Ameuepusha moyo wake na dini Yake? Na yoyote ambaye Allah Mtukufu Ameacha kumuafikia kufuata dini Yake na yale Aliyoyaamrisha, basi hana njia ya kufikia kwenye uongofu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net