Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 4 · Aya ya 89

An-Nisaa 4:89

النساء

وَدُّوا۟ لَوْ تَكْفُرُونَ كَمَا كَفَرُوا۟ فَتَكُونُونَ سَوَآءً ۖ فَلَا تَتَّخِذُوا۟ مِنْهُمْ أَوْلِيَآءَ حَتَّىٰ يُهَاجِرُوا۟ فِى سَبِيلِ ٱللَّهِ ۚ فَإِن تَوَلَّوْا۟ فَخُذُوهُمْ وَٱقْتُلُوهُمْ حَيْثُ وَجَدتُّمُوهُمْ ۖ وَلَا تَتَّخِذُوا۟ مِنْهُمْ وَلِيًّا وَلَا نَصِيرًا

Maana

Wanapenda lau kuwa mtakufuru kama walivyokufuru wao, ili muwe sawasawa. Basi, msifanye marafiki wandani miongoni mwao mpaka wahame kwenda katika njia ya Mwenyezi Mungu. Na wakigeuka, basi wakamateni, na waueni popote mnapowapata. Wala msifanye miongoni mwao rafiki mwandani wala msaidizi.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Wanapenda lau kuwa nanyi mnge kufuru kama walivyo kufuru wao, ili muwe sawa sawa. Basi msiwafanye marafiki miongoni mwao mpaka wahame kwa ajili ya Dini ya Mwenyezi Mungu. Na wakikengeuka basi wakamateni na wauweni popote mnapo wapata. Wala msimfanye rafiki katika wao wala msaidizi. [89]

[89] Hakika nyinyi mnapenda kuwaongoa hawa wanaafiki, na wao wanapenda nyinyi mkufuru kama wao, ili muwe nyote sawa kwa ukafiri. Ilivyo kuwa hivyo basi msitake wa kukuungeni mkono miongoni mwao. Wala msiwafanye wenzenu, mpaka wakubali kutoka huko kwao kuwania Jihadi kwa ajili ya Uislamu. Hivyo tu ndio itawatoka sifa ya unaafiki. Lakini wakiyakataa hayo, wakaungana na maadui zenu, basi wauweni popote mtapo wapata, wala msiwaone kuwa ni wenzenu, wala msiwachukulie kuwa ndio wasaidizi wenu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hawa wanafiki waliwatamania nyinyi Waumini lau mngekanusha uhakika wa lile ambalo nyoyo zenu zimeliamini kama vile wao walivyolikanusha kwa nyoyo zao, ili muwe sawa na wao katika kukanusha. Basi msiwafanye ni wasafiwa wenu mpaka wahame katika njia ya Allah Mtukufu kama ushahidi wa ukweli wa Imani yao. Basi wakiyakataa yale waliyolinganiwa kwayo, washikeni popote waliopo na muwaue, wala msimfanye yoyote katika wao kuwa ni msimamizi badala ya Allah Mtukufu wala ni mwokozi ambaye mnataka awaokoe.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Nisaa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net