Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 4 · Aya ya 87

An-Nisaa 4:87

النساء

ٱللَّهُ لَآ إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۚ لَيَجْمَعَنَّكُمْ إِلَىٰ يَوْمِ ٱلْقِيَـٰمَةِ لَا رَيْبَ فِيهِ ۗ وَمَنْ أَصْدَقُ مِنَ ٱللَّهِ حَدِيثًا

Maana

Mwenyezi Mungu, hapana mungu isipokuwa Yeye. Kwa yakini, atawakusanya Siku ya Kiyama. Halina shaka hilo. Na ni nani mkweli zaidi katika mazungumzo kuliko Mwenyezi Mungu?

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Mwenyezi Mungu, hapana mungu isipo kuwa Yeye. Kwa yakini atakukusanyeni Siku ya Kiyama. Halina shaka hilo. Na ni nani msema kweli kuliko Mwenyezi Mungu? [87]

[87] Mwenyezi Mungu ambaye hapana mungu ila Yeye, wala hapana mwenye uweza ila Yeye, hapana shaka atakufufueni baada ya kufa kwenu, na atakukusanyeni kwenye kituo cha kuhisabiwa kwa ajili ya malipo. Hayo hayana shaka. Yeye anasema hayo, basi msiyatilie shaka maneno yake. Na kauli gani iliyo ya kweli zaidi kuliko kauli ya Mwenyezi Mungu?

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Allah Mtukufu, Peke Yake, Aliyepwekeka kwa uungu wa viumbe wote, Ndiye Atakayewakusanya nyinyi Siku ya Kiyama isiyokuwa na shaka, kwa kuhesabiwa na kulipwa. Na hakuna yoyote mkweli zaidi wa maneno anayoyatolea habari kuliko Allah Mtukufu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Nisaa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net