Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 4 · Aya ya 86

An-Nisaa 4:86

النساء

وَإِذَا حُيِّيتُم بِتَحِيَّةٍ فَحَيُّوا۟ بِأَحْسَنَ مِنْهَآ أَوْ رُدُّوهَآ ۗ إِنَّ ٱللَّهَ كَانَ عَلَىٰ كُلِّ شَىْءٍ حَسِيبًا

Maana

Na mnapoamkiwa kwa maamkizi yoyote, basi itikieni kwa yaliyo mazuri zaidi kuliko hayo, au yarejesheni hayo hayo. Hakika, Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuhesabu kila kitu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na mnapo amkiwa kwa maamkio yoyote, basi nanyi itikieni kwa yaliyo bora kuliko hayo, au rejesheni hayo hayo. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuhisabu kila kitu. [86]

[86] Akikuamkieni mtu yeyote kwa maamkio ya salamu, au dua, au ya namna yoyote ya hishima, au namna nyengine yoyote ile, basi mjibuni kwa maamkio yaliyo mazuri zaidi, au kwa uchache mjibuni kama alivyo kuamkieni yeye. Kwani hakika Mwenyezi Mungu ni mwenye kutia hisabuni kila kitu, kikubwa na kidogo.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na Muislamu akiwatolea salamu, muitikieni kwa maneno mazuri zaidi na kwa furaha zaidi, au muitikieni salamu kama vile alivyowatolea. Na kila mmoja ana thawabu zake na malipo yake. Hakika Allah Mtukufu ni mwenye kulipa kwa kila kitu (mnachokifanya).

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Nisaa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net