Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 4 · Aya ya 85

An-Nisaa 4:85

النساء

مَّن يَشْفَعْ شَفَـٰعَةً حَسَنَةً يَكُن لَّهُۥ نَصِيبٌ مِّنْهَا ۖ وَمَن يَشْفَعْ شَفَـٰعَةً سَيِّئَةً يَكُن لَّهُۥ كِفْلٌ مِّنْهَا ۗ وَكَانَ ٱللَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَىْءٍ مُّقِيتًا

Maana

Mwenye kufanya uombezi mzuri, ana fungu lake katika hayo. Na mwenye kufanya uombezi mbaya, naye ana sehemu yake katika hayo. Na hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye uwezo na ujuzi juu ya kila kitu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Mwenye kusaidia msaada mwema ana fungu lake katika hayo, na mwenye kusaidia msaada mwovu naye ana sehemu yake katika hayo. Na hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye uweza na ujuzi juu ya kila kitu. [85]

[85] Na hawa wanaafiki husaidia ufisadi, na watu wa Imani husaidia Haki. Na mwenye kusaidia jambo jema ana fungu lake la thawabu. Na mwenye kuwasaidia watu waovu naye ana mzigo wake wa dhambi katika malipo yake. Na Mwenyezi Mungu ana uweza juu ya kila kitu, na Mwenye kujua kila kitu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Mwenye kumshughulikia mwingine apate mema, atapata fungu la thawabu kwa huko kuingilia kwake kati. Na mwenye kujishughulisha juu ya kumdhuru mwingine, Atapata fungu la mzigo wa dhambi. Na Allah Mtukufu ni Shahidi na ni Mtunzi wa kila jambo.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Nisaa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net