Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 4 · Aya ya 84

An-Nisaa 4:84

النساء

فَقَـٰتِلْ فِى سَبِيلِ ٱللَّهِ لَا تُكَلَّفُ إِلَّا نَفْسَكَ ۚ وَحَرِّضِ ٱلْمُؤْمِنِينَ ۖ عَسَى ٱللَّهُ أَن يَكُفَّ بَأْسَ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ ۚ وَٱللَّهُ أَشَدُّ بَأْسًا وَأَشَدُّ تَنكِيلًا

Maana

Basi pigana vita katika Njia ya Mwenyezi Mungu. Hutwikwi isipokuwa nafsi yako tu. Na wahimize Waumini. Huenda Mwenyezi Mungu akayazuia mashambulizi ya wale waliokufuru. Na Mwenyezi Mungu ndiye Mkali zaidi wa kushambulia, na Mkali zaidi wa kutesa.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Basi pigana katika Njia ya Mwenyezi Mungu. Hukalifishwi ila nafsi yako tu. Na wahimize Waumini. Huenda Mwenyezi Mungu akayazuia mashambulio ya walio kufuru. Na Mwenyezi Mungu ndiye Mkali zaidi wa kushambulia na Mkali zaidi wa kuadhibu. [84]

[84] Na kama wapo kati yenu mfano wa hawa wanaafiki basi wapuuzilie mbali. Na wewe pigana kwa ajili ya Neno la Mwenyezi Mungu na kwa ajili ya Haki. Wewe huna jukumu ila la nafsi yako tu. Kisha waite Waumini wende vitani, na wahimize. Huenda Mwenyezi Mungu kwa kupitia kwako na kwao akazuia hayo mashambulio ya makafiri. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kukuungeni mkono, na ni Mwenye kukunusuruni. Na Yeye ana nguvu kuliko wote, na mkali kuliko wote katika kuwaadhibu makafiri.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Basi pigana jihadi, ewe Nabii, katika njia ya Allah Mtukufu na kulitukuza neno Lake. Hulazimishwi kitendo cha asiyekuwa wewe wala hutaadhibiwa kwacho. Na wahimize Waumini kupigana jihadi na uwavutie wafanye hivyo, kwani huenda Allah Mtukufu Akazuia, kwa ajili yako na wao, mashambulizi ya makafiri na nguvu zao. Na Allah Mtukufu Ana nguvu nyingi zaidi na Ana adhabu kubwa zaidi kwa makafiri.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Nisaa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net