An-Nisaa 4:83
النساءوَإِذَا جَآءَهُمْ أَمْرٌ مِّنَ ٱلْأَمْنِ أَوِ ٱلْخَوْفِ أَذَاعُوا۟ بِهِۦ ۖ وَلَوْ رَدُّوهُ إِلَى ٱلرَّسُولِ وَإِلَىٰٓ أُو۟لِى ٱلْأَمْرِ مِنْهُمْ لَعَلِمَهُ ٱلَّذِينَ يَسْتَنۢبِطُونَهُۥ مِنْهُمْ ۗ وَلَوْلَا فَضْلُ ٱللَّهِ عَلَيْكُمْ وَرَحْمَتُهُۥ لَٱتَّبَعْتُمُ ٱلشَّيْطَـٰنَ إِلَّا قَلِيلًا
Na linapowajia jambo lolote linalohusiana na amani au hofu, wao wanalitangaza. Na lau kuwa wangelipeleka hilo kwa Mtume na kwa wenye mamlaka kati yao, wale wanaochunguza miongoni mwao wangelijua. Na lau kuwa si fadhila ya Mwenyezi Mungu juu yenu na rehema yake, mngelimfuata Shetani isipokuwa wachache tu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na linapo wafikia jambo lolote lilio khusu amani au la kitisho wao hulitangaza. Na lau kuwa wangeli lipeleka kwa Mtume na kwa wenye mamlaka kati yao, wale wanao chunguza wangeli lijua. Na lau kuwa si fadhila ya Mwenyezi Mungu juu yenu na rehema yake mngeli mfuata Shet'ani ila wachache wenu tu. [83]
[83] Na hichi kikundi cha wanaafiki kikipata khabari zozote zilio khusu nguvu au udhaifu wa Waislamu huzitangaza na kuzieneza nje, ili kuwababaisha Waislamu au kuwatia khofu katika nyoyo zao, au ili zifike khabari zao kwa maadui wao. Na lau kuwa hawa wanaafiki watangazao wamerudisha jambo lilio kuhusu usalama au kitisho kwa Mtume na kwa wakuu wa mambo miongoni mwa waongozi na Masahaba wakubwa, wakataka kwao kujua hakika, wangeli jua hao wanao jitahidi kuchungua mambo na kuyatangaza, kuwa yaliyo kweli yanatokana na Mtume na waongozi wengine. Na lau kuwa si fadhila ya Mwenyezi Mungu juu yenu kwa alivyo zithibitisha nyoyo zenu juu ya Imani, na kuzuia fitina, na rehema yake kwa kukupeni sababu na njia za ushindi, wengi wenu wangeli fuata upotovu wa Shetani, na wasingeli okoka kutokana na upotovu wake ila wachache tu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na likiwajia, hawa ambao Imani haijakita ndani ya nyoyo zao, jambo ambalo inapasa lifichwe linalofungamana na usalama, ambao heri yake itarudi kwa Uislamu na Waislamu, au hofu, ambayo inatia babaiko ndani ya nyoyo zao, wanalitoa nje na kulitangaza kwa watu. Na lau wao wangelipeleka, lile liliowajia, kwa Mtume wa Allah Mtukufu, rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie na kwa wenye ujuzi na ufahamu, wangaliujua uhakika wake wale wachambuzi kati yao. Na lau si Allah Mtukufu kuwafanyia wema na kuwaonea huruma, Mungalimfuata Shetani na mawazo mnayotiwa naye, isipokuwa wachache katika nyinyi.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net