Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 4 · Aya ya 82

An-Nisaa 4:82

النساء

أَفَلَا يَتَدَبَّرُونَ ٱلْقُرْءَانَ ۚ وَلَوْ كَانَ مِنْ عِندِ غَيْرِ ٱللَّهِ لَوَجَدُوا۟ فِيهِ ٱخْتِلَـٰفًا كَثِيرًا

Maana

Kwani hawaizingatii hii Qur-ani? Na lau kuwa ingetoka kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu, bila ya shaka wangelikuta ndani yake hitilafu nyingi.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Hebu hawaizingatii hii Qur'ani? Na lau kuwa imetoka kwa asiye kuwa Mwenyezi Mungu bila ya shaka wangeli kuta ndani yake khitilafu nyingi. [82]

[82] Basi hao wanaafiki hawakizingatii Kitabu cha Mwenyezi Mungu wakajua hoja za Mwenyezi Mungu zilio juu yao kuwa ni waajibu kut'ii na kufuata amri yako? Na kwamba Kitabu hichi kinatoka kwa Mwenyezi Mungu kwa yalivyo shikamana maana yake na hukumu zake, na kinavyo fungamana wenyewe kwa wenyewe? Hii ni dalili kuwa ni kweli kinatoka kwa Mwenyezi Mungu; kwani lau kuwa kinatokana na mwenginewe basi maana yake yangeli gongana, na hukumu zake zingeli khitalifiana sana.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Kwani hawa hawaiangalii Qur’ani na haki iliyokuja nayo, kwa kuitaamali na kuizingatia, namna ilivyokuja kwa utaratibu uliopangika unaomfanya mtu awe na yakini kuwa inatoka kwa Allah Mtukufu Peke Yake? Na lau yangekuwa yatoka kwa asiyekuwa Yeye, wangalipata ndani yake tafauti kubwa.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Nisaa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net