Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 4 · Aya ya 81

An-Nisaa 4:81

النساء

وَيَقُولُونَ طَاعَةٌ فَإِذَا بَرَزُوا۟ مِنْ عِندِكَ بَيَّتَ طَآئِفَةٌ مِّنْهُمْ غَيْرَ ٱلَّذِى تَقُولُ ۖ وَٱللَّهُ يَكْتُبُ مَا يُبَيِّتُونَ ۖ فَأَعْرِضْ عَنْهُمْ وَتَوَكَّلْ عَلَى ٱللَّهِ ۚ وَكَفَىٰ بِٱللَّهِ وَكِيلًا

Maana

Na wanasema: 'Tunatii.' Lakini wanapotoka kule uliko, kundi moja miongoni mwao hupanga njama usiku kinyume na unayoyasema. Na Mwenyezi Mungu anayaandika yote hayo wanayoyapangia njama za usiku. Basi wape mgongo, na umtegemee Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu anatosha kuwa Mtegemewa.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na wanasema: Tunat'ii. Lakini wanapo toka kwako kundi moja miongoni mwao hupanga njama usiku kinyume na unayo yasema. Na Mwenyezi Mungu anayaandika yote hayo wanayo yapangia njama za usiku. Basi waachilie mbali, na umtegemee Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu ni Mtegemewa wa kutosha. [81]

[81] Na kikundi hichi kinacho tapatapa husema: Amri yako tunait'ii. Hatuna kwako ila kut'ii unayo amrisha na kukataza. Lakini wakisha toka kwako wakawa mbali nawe, baadhi yao hupanga vijambo vyao usiku usiku, kinyume na unavyo waambia ya kuwaamrisha na kuwakataza. Na Mwenyezi Mungu, Subhanahu wa Taa'la, Aliye takasika na Kutukuka, anayadhibiti yote wanayo yapanga kwa siri. Basi usiwashughulikie, na wapuuze, na mwachie mambo yao Mwenyezi Mungu, na wewe mtegemee Yeye. Na Mwenyezi Mungu ni wa kutosha kuwa ni Mtegemewa wako, na Mlinzi wako wa kumwachilia mambo yako yote.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na hawa wenye kukataa, wakiwa kwenye baraza ya Mtume, rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukiye, wanajidhihirisha kuwa wanamtii Mtume na kuyafuata yale aliyokuja nayo, na wakiwa mbali na yeye na wakaondoka kwenye baraza yake, linatoka kundi katika wao likapanga njama kinyume cha yale waliyoyadhihirisha ya kumtii. Na wao hawakujua kwamba Allah Mtukufu Anadhibiti hesabu ya yale wanayoyapanga na kwamba Yeye Atawalipa kwa hayo malipo kamili. Basi wape mgongo na usiwajali, kwani wao hawatakudhuru. Na tegemea kwa Allah Mtukufu, kwani yeye Peke Yake Ndiye Mwenye kukutosha kwa usimamizi na utetezi.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Nisaa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net