Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 4 · Aya ya 80

An-Nisaa 4:80

النساء

مَّن يُطِعِ ٱلرَّسُولَ فَقَدْ أَطَاعَ ٱللَّهَ ۖ وَمَن تَوَلَّىٰ فَمَآ أَرْسَلْنَـٰكَ عَلَيْهِمْ حَفِيظًا

Maana

Mwenye kumtii Mtume, basi hakika amemtii Mwenyezi Mungu. Na mwenye kugeuka, basi Sisi hatukukutuma uwe mlinzi juu yao.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Mwenye kumt'ii Mtume basi ndio amemt'ii Mwenyezi Mungu. Na anaye kengeuka, basi Sisi hatukukutuma wewe uwe ni mlinzi wao. [80]

[80] Mwenye kumt'ii Mtume basi ndio amemt'ii Mwenyezi Mungu, kwani yeye haamrishi ila alicho amrisha Mwenyezi Mungu. Wala hakatazi ila alicho kataza Mwenyezi Mungu. Kwa hivyo kumt'ii yeye (Mtume s.a.w.) ndio kutenda na kuacha kwa ut'iifu wa Mwenyezi Mungu. Na mwenye kukataa kukut'ii wewe basi, kwani Sisi hatukukupeleka wewe ila uwe ni mbashiri na mwonyaji tu, sio uwe ni mlinzi wao na muangalizi wao, uwalindie vitendo vyao. Hayo ni yetu Sisi sio yako.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Yoyote mwenye kumkubali Mtume, rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukiye, na akafuata uongofu wake kivitendo, basi amemkubali Allah Mtukufu na amefuata amri Yake. Na yoyote aliyekataa kumtii Allah Mtukufu na Mtume Wake, basi hatukukutumiliza, ewe Mtume, kwa hawa wenye kukataa uwe ni mtunzi wa kuyadhibiti matendo yao na kuwahesabu kwa hayo. Hesabu yao ni juu yetu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Nisaa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net