An-Nisaa 4:79
النساءمَّآ أَصَابَكَ مِنْ حَسَنَةٍ فَمِنَ ٱللَّهِ ۖ وَمَآ أَصَابَكَ مِن سَيِّئَةٍ فَمِن نَّفْسِكَ ۚ وَأَرْسَلْنَـٰكَ لِلنَّاسِ رَسُولًا ۚ وَكَفَىٰ بِٱللَّهِ شَهِيدًا
Yaliyokupata katika mazuri, basi ni kutokana na Mwenyezi Mungu. Na yaliyokusibu katika maovu, basi ni kutokana na nafsi yako. Nasi tumekutuma kwa watu uwe ni Mtume. Na Mwenyezi Mungu anatosha kuwa Shahidi.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Jema lilio kufikia limetokana na Mwenyezi Mungu. Na ovu lilio kusibu linatokana na nafsi yako. Nasi tumekutuma kwa watu uwe ni Mtume. Na Mwenyezi Mungu ni shahidi wa kutosha. [79]
[79] Ewe Nabii! Kufanikiwa, na neema, na afya, na salama unayo ipata inatokana na fadhila ya Mwenyezi Mungu juu yako. Yeye anafanya haya kukufadhili kukufanyia hisani. Na inapo kusibu shida, na mashaka, na udhiya, na ya karaha, basi yanatokana na nafsi yako mwenyewe kwa sababu ya upungufu fulani au makosa uliyo yatenda. Haya anaambiwa Mtume s.a.w. ni kama mfano wa wanaadamu wote ijapo kuwa halikutokea kwake la uovu. Kwani Mtume anaambiwa: Tumekutuma kuwa Mtume kutoka kwetu kwa watu wote. Na Mwenyezi Mungu ni shahidi wa kufikisha kwako huo ujumbe na juu ya kuitikia kwao hao watu. Na Yeye ni Mjuzi wa kutosha.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Chochote kinachokupata, ewe binadamu, cha wema na neema, kinatoka kwa Allah Mtukufu, Peke Yake, kwa ukarimu na hisani. Na chochote kinachokufika cha tabu na mashaka ni kwa sababu ya vitendo vyako vibaya na makosa na madhambi yaliyotendwa na mikono yako miwili. Na tumekutumiliza, ewe Mtume, kuwa ni Mtume kwa watu wote uwafikishie ujumbe wa Mola wako. Na inatosha kuwa Allah Mtukufu ni shahidi juu ya ukweli wa utume Wako.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net