Ruka hadi kwenye maudhui
Tafsir As-Saadi - Swahili · An-Nisaa
Sura ya 4

An-Nisaa

Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.

Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22

Aya ya 85

مَّن يَشْفَعْ شَفَـٰعَةً حَسَنَةً يَكُن لَّهُۥ نَصِيبٌ مِّنْهَا ۖ وَمَن يَشْفَعْ شَفَـٰعَةً سَيِّئَةً يَكُن لَّهُۥ كِفْلٌ مِّنْهَا ۗ وَكَانَ ٱللَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَىْءٍ مُّقِيتًا 85

{85} Na kinachokusudiwa na uombezi hapa ni kusaidiana katika jambo miongoni mwa mambo. Kwa hivyo, mwenye kumwombea mwengine uombezi na akasimama pamoja naye katika jambo la heri, ikiwemo ndani yake kuwaombea wanaodhulumiwa kwa anayewadhulumu, basi atakuwa na fungu katika uombezi wake kulingana na juhudi yake, na matendo yake, na manufaa yake, na wala hakipunguki kitu katika malipo ya mtu wa asili au wa moja kwa moja. Na mwenye kumsaidia mwingine katika kufanya jambo baya, basi anapata sehemu ya dhambi kulingana na kile alichokifanya na kusaidia katika hilo. Na katika hili kuna himizo kubwa juu ya kushirikiana katika wema na uchamungu, na kukemea kukubwa dhidi ya kushirikiana katika dhambi na kupita mipaka. Na alilithibitisha hilo kwa kauli yake. “Na hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye uwezo na ujuzi juu ya kila kitu.” Yani ni shahidi, mwenye kuhifadhi, mwenye kuhesabu matendo haya, na atamlipa kila mtu yale anayoyastahiki.