Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 4 · Aya ya 8

An-Nisaa 4:8

النساء

وَإِذَا حَضَرَ ٱلْقِسْمَةَ أُو۟لُوا۟ ٱلْقُرْبَىٰ وَٱلْيَتَـٰمَىٰ وَٱلْمَسَـٰكِينُ فَٱرْزُقُوهُم مِّنْهُ وَقُولُوا۟ لَهُمْ قَوْلًا مَّعْرُوفًا

Maana

Na wakihudhuria ugawi (wa mali ya urithi) jamaa wa karibu, na mayatima, na masikini, basi wapeni kwayo, na waambieni kauli njema.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na wakati wa kugawanya wakihudhuria jamaa na mayatima na masikini, wapeni katika hayo mali ya urithi, na semeni nao maneno mema. [8]

[8] Na pindi ikiwa wamehudhuria wakati ule wa kugawanya urithi baadhi ya jamaa ambao hawarithi, na ni mayatima na masikini, basi wakirimuni kwa kuwapa chochote katika huo urithi ili kuzipoza nafsi zao, na kuondoa uhasidi katika nyoyo zao. Na ni vizuri pia katika kuwapa kuleta maneno laini na udhuru mwema.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Watakapohudhuria kikao cha kugawanywa urithi, jamaa wa maiti wa karibu wasiokuwa na haki ya kurithi au waliofiwa na baba zao nao ni wadogo au wasiokuwa na mali, basi wapeni chochote katika mali hayo, kwa njia ya kuwapoza, kabla mali hayajagawanywa kwa wenyewe. Na waambieni neno zuri lisilokuwa chafu wala baya.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Nisaa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net