An-Nisaa 4:7
النساءلِّلرِّجَالِ نَصِيبٌ مِّمَّا تَرَكَ ٱلْوَٰلِدَانِ وَٱلْأَقْرَبُونَ وَلِلنِّسَآءِ نَصِيبٌ مِّمَّا تَرَكَ ٱلْوَٰلِدَانِ وَٱلْأَقْرَبُونَ مِمَّا قَلَّ مِنْهُ أَوْ كَثُرَ ۚ نَصِيبًا مَّفْرُوضًا
Wanaume wana fungu katika yale wanayoyaacha wazazi na jamaa wa karibu. Na wanawake wanalo fungu katika yale waliyoyaacha wazazi na jamaa wa karibu. Kwa kile kilicho kidogo chake au kingi. Ni mafungu yaliyofaradhiwa.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Wanaume wana sehemu katika wanayo yaacha wazazi na jamaa walio karibia. Na wanawake wanayo sehemu katika waliyo yaacha wazazi na jamaa walio karibia. Ikiwa kidogo au kingi. Hizi ni sehemu zilizo faridhiwa. [7]
[7] Wanaume wanalo fungu lao katika mali waliyo yaacha kurithiwa wazazi wawili na jamaa walio karibia. Na wanawake, aidha, wana fungu lao, bila ya kunyimwa au kupunjwa. Na mafungu hayo yamethibiti, na yamefaridhiwa, na yamekadiriwa, yakiwa mali yenyewe kidogo au mengi.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Wanaume, wadogo na wakubwa, wana fungu lililopasishwa na Allah Mtukufu katika mali yalioachwa na wazazi wawili au jamaa wa karibu, yawe ni kidogo mali hayo au ni mengi, katika mafungu maalumu yaliyo wazi yaliyofaradhiwa na Allah Mtukufu, Aliyetukuka na kushinda, kwa hawa wanaume na pia wanawake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net