An-Nisaa 4:9
النساءوَلْيَخْشَ ٱلَّذِينَ لَوْ تَرَكُوا۟ مِنْ خَلْفِهِمْ ذُرِّيَّةً ضِعَـٰفًا خَافُوا۟ عَلَيْهِمْ فَلْيَتَّقُوا۟ ٱللَّهَ وَلْيَقُولُوا۟ قَوْلًا سَدِيدًا
Na wachelee wale ambao lau kuwa na wao wangeliacha nyuma yao dhuria wanyonge, wangeliwahofia. Basi nao wamche Mwenyezi Mungu, na waseme kauli iliyo sawa.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na wachelee wale ambao lau kuwa na wao wangeli acha nyuma yao watoto wanyonge wangeli wakhofia. Basi nao wamche Mwenyezi Mungu, na waseme maneno yaliyo sawa. [9]
[9] Watu watahadhari na kuwadhulumu mayatima, na wawaogopee watoto wao wanyonge wasije na wao wakadhulumiwa kwa watendavyo wazee kwa mayatima wa watu wengine. Na wamwogope Mwenyezi Mungu katika kuwatendea mayatima. Na waseme maneno yaliyo kaa sawa yanayo fuata haki, wala wasimdhulumu yeyote.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na waogope wale ambao lau watakufa na wataacha nyuma yao watoto wadogo madhaifu, wakawachelea dhuluma na kupotea, basi na wamche Allah Mtukufu juu ya wale mayatima na wengineo walio chini ya mikono yao. Nako ni kuwahifadhia mali yao, kuwalea vizuri na kuwaondolea ya kuwaudhi. Na wawaambie maneno yanayolingana na usawa na wema.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net