An-Nisaa 4:10
النساءإِنَّ ٱلَّذِينَ يَأْكُلُونَ أَمْوَٰلَ ٱلْيَتَـٰمَىٰ ظُلْمًا إِنَّمَا يَأْكُلُونَ فِى بُطُونِهِمْ نَارًا ۖ وَسَيَصْلَوْنَ سَعِيرًا
Hakika, wale wanaokula mali za mayatima kwa dhuluma, hakuna shaka yoyote wanakula moto matumboni mwao. Na wataingia Moto wenye mwako mkali.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hakika wanao kula mali ya mayatima kwa dhulma, hapana shaka yoyote wanakula matumboni mwao moto, na wataingia Motoni. [10]
[10] Hakika wanao wadhulumu mayatima kwa kuchukua mali yao bila ya haki, hakika wanakula yatakayo wapelekea Motoni. Na Mwenyezi Mungu atawaadhibu Siku ya Kiyama kwa moto mkali wenye kutia machungu.(Je, huwaje basi adhabu ya mwenye kudhulumu mali ya Mwenyezi Mungu? Wakfu za misikiti, madrasa n.k.? Na huwaje mwenye kuuwa ili apate kudhulumu mali ya mayatima wa hao alio wauwa?)
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Wale wanaozifuja mali za mayatima wakawa wazichukua pasi na haki, hakika wanakula Moto utakaowaka matumboni mwao Siku ya Kiyama; wataungia Moto ambao watalisikia joto lake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net