Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 4 · Aya ya 64

An-Nisaa 4:64

النساء

وَمَآ أَرْسَلْنَا مِن رَّسُولٍ إِلَّا لِيُطَاعَ بِإِذْنِ ٱللَّهِ ۚ وَلَوْ أَنَّهُمْ إِذ ظَّلَمُوٓا۟ أَنفُسَهُمْ جَآءُوكَ فَٱسْتَغْفَرُوا۟ ٱللَّهَ وَٱسْتَغْفَرَ لَهُمُ ٱلرَّسُولُ لَوَجَدُوا۟ ٱللَّهَ تَوَّابًا رَّحِيمًا

Maana

Na hatukumtuma Mtume yeyote isipokuwa atiiwe kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Na lau pale walipozidhulumu nafsi zao, wangelikujia, wakamwomba Mwenyezi Mungu kuwafutia dhambi, na Mtume akawaombea kufutiwa dhambi, basi bila ya shaka wangelimkuta Mwenyezi Mungu ni Mwenye kupokea toba, Mwenye kurehemu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na hatukumtuma Mtume yeyote ila at'iiwe kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Na lau pale walipo jidhulumu nafsi zao wangeli kujia, wakamwomba Mwenyezi Mungu msamaha, na Mtume akawaombea msamaha, hapana shaka wangeli mkuta Mwenyezi Mungu ni Mwenye kupokea toba na Mwenye kurehemu. [64]

[64] Na Sisi hatukumtuma Mtume yeyote ila jambo lake kuu ni kuwa at'iiwe, na ut'iifu huo ni kwa ruhusa iliyo toka kwa Mwenyezi Mungu. Na hakika mwenye kwenda kinyume, au kukanusha, au kukhaalifu, anakuwa ni mwenye kujidhulumu mwenyewe. Na lau kuwa hawa walio jidhulumu wakirejea kwenye uwongofu, wakakujia wakiomba msamaha kutokana na Mwenyezi Mungu kwa yale waliyo yatenda, na wewe ukawaombea msamaha kwa mujibu wa ujumbe wako na kwa ulivyo ona ilivyo geuka hali yao, basi hapana shaka watamkuta Mwenyezi Mungu, Aliye takasika na kutukuka, ni Mwingi wa kukubali toba, na Mwenye kuwarehemu waja wake.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hatukumtumiliza Mtume yoyote, miongoni mwa Mitume wetu, isipokuwa ni afuatwe kwa amri ya Allah Mtukufu na uamuzi Wake. Na lau kwamba hawa waliojidhulumu nafsi zao kwa kutenda mabaya, wangekujia, ewe Mtume, katika uhai wako, hali ya kutubia na kumuomba Allah Mtukufu Awasamehe madhambi yao, nawe ukawaombea msamaha, wangalimkuta Allah Mtukufu ni Mwingi wa kukubali toba, ni Mwingi wa kurehemu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Nisaa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net