An-Nisaa 4:63
النساءأُو۟لَـٰٓئِكَ ٱلَّذِينَ يَعْلَمُ ٱللَّهُ مَا فِى قُلُوبِهِمْ فَأَعْرِضْ عَنْهُمْ وَعِظْهُمْ وَقُل لَّهُمْ فِىٓ أَنفُسِهِمْ قَوْلًۢا بَلِيغًا
Hao ndio wale ambao Mwenyezi Mungu anayajua yaliyo katika nyoyo zao. Basi wapuuze, na uwawaidhi, na uwaambie maneno ya kuathiri na kuingia katika nafsi zao.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hao ndio wale ambao Mwenyezi Mungu anayajua yaliyomo ndani ya nyoyo zao. Basi waachilie mbali, uwape mawaidha na uwaambie maneno ya kuathiri na kuingia katika nafsi zao. [63]
[63] Hao ndio wanao kula yamini kuwa hawakutaka ila wema na vitendo vya muwafaka. Mwenyezi Mungu anayajua vyema yaliyomo katika nyoyo zao, na anaujua uwongo wa hiyo kauli yao. Basi wewe usishughulike na maneno yao. Waite kwenye haki kwa mawaidha yaliyo mema, na sema nao maneno yenye hikima yenye kuathiri yanayo fika ndani ya nyoyo zao.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hao ndio ambao Allah Mtukufu Anaujua uhakika unafiki ulio ndani ya nyoyo zao. Basi jiepushe nao, uwaonye ubaya wa mambo waliyonayo na uwaambie maneno yenye kuwaathiri kwa njia ya kuwakemea.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net