An-Nisaa 4:62
النساءفَكَيْفَ إِذَآ أَصَـٰبَتْهُم مُّصِيبَةٌۢ بِمَا قَدَّمَتْ أَيْدِيهِمْ ثُمَّ جَآءُوكَ يَحْلِفُونَ بِٱللَّهِ إِنْ أَرَدْنَآ إِلَّآ إِحْسَـٰنًا وَتَوْفِيقًا
Basi inakuwa vipi unapowasibu msiba kwa sababu ya yale iliyotanguliza mikono yao? Hapo, wanakujia wakiapa kwa Mwenyezi Mungu wakisema: Hatukutaka isipokuwa wema na mapatano.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Basi inakuwaje unapo wasibu msiba kwa sababu ya yale iliyo tanguliza mikono yao? Hapo tena hukujia wakiapa kwa Mwenyezi Mungu wakisema: Hatukutaka ila wema na mapatano. [62]
[62] Itakuwaje hali basi yakiwateremkia masaibu kwa sababu ya uovu wao na upotovu wa vitendo vyao, na wasipate pa kukimbilia ila kwako! Hapo basi watakuapia Mungu mbele yako kuwa wao hawakukusudia kwa maneno yao na vitendo vyao ila wema tu na kutaka mapatano.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hali ya wanafiki hawa itakuwa namna gani, watakapofikiwa na misiba kwa sababu ya makosa yaliyotendwa na mikono yao kisha wakakujia, ewe Mtume, wakitoa udhuru na kukuhakikishia kwamba wao hawakuwa na malengo yoyote, kwa matendo yao hayo, isipokuwa ni kutenda wema na kuleta upatanishi baina ya wagomvi?
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net