Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 4 · Aya ya 61

An-Nisaa 4:61

النساء

وَإِذَا قِيلَ لَهُمْ تَعَالَوْا۟ إِلَىٰ مَآ أَنزَلَ ٱللَّهُ وَإِلَى ٱلرَّسُولِ رَأَيْتَ ٱلْمُنَـٰفِقِينَ يَصُدُّونَ عَنكَ صُدُودًا

Maana

Na wanapoambiwa: 'Njooni kwa yale aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu na kwa Mtume', utawaona wanafiki wanaepukana na wewe kuepuka kukubwa.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na wanapo ambiwa: Njooni kwenye yale aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu, na njooni kwa Mtume; utawaona wanaafiki wanakukwepa kwa upinzani. [61]

[61] Na wakiambiwa: Njooni kwenye Qur'ani na Sharia aliyo iteremsha Mwenyezi Mungu, na njooni kwa Mtume wake akubainishieni, utaona hao wanaafiki wanajitenga nawe kabisa wanakukataa.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na hawa wanaponasihiwa na kuambiwa, «Njooni kwenye yale yaliyoateremshwa na Allah Mtukufu na kwa Mtume na uongofu wake», utawaona wale wenye kudhihirisha Imani na kuficha ukafiri, wanakugeuka na kukupa mgongo.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Nisaa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net