An-Nisaa 4:60
النساءأَلَمْ تَرَ إِلَى ٱلَّذِينَ يَزْعُمُونَ أَنَّهُمْ ءَامَنُوا۟ بِمَآ أُنزِلَ إِلَيْكَ وَمَآ أُنزِلَ مِن قَبْلِكَ يُرِيدُونَ أَن يَتَحَاكَمُوٓا۟ إِلَى ٱلطَّـٰغُوتِ وَقَدْ أُمِرُوٓا۟ أَن يَكْفُرُوا۟ بِهِۦ وَيُرِيدُ ٱلشَّيْطَـٰنُ أَن يُضِلَّهُمْ ضَلَـٰلًۢا بَعِيدًا
Je, hukuwaona wale wanaodai kwamba wameamini yale yaliyoteremshwa kwako na yale yaliyoteremshwa kabla yako? Wanataka kupeleka kesi yao kwa Twaghut, na ilhali kwa hakika waliamrishwa kwamba wazikufuru! Na anataka Shetani kwamba awapoteze kupotea kwa mbali.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Huwaoni wale wanao dai kwamba wameamini yale yaliyo teremshwa kwako na yaliyo teremshwa kabla yako? Wanataka wakahukumiwe kwa njia ya upotofu, na hali wameamrishwa wakatae hayo! Na Shet'ani anataka kuwapotezelea mbali. [60]
[60] Ewe Nabii! Huwastaajabii hao wanao dai kuwa wanasadiki Kitabu ulicho teremshiwa wewe na vilivyo teremshwa kabla yako wewe, wanataka wahukumiwe katika ugomvi wao kwenye upotovu na uharibifu na hukumu isiyo kuwa ya Mwenyezi Mungu? Na Mwenyezi Mungu amekwisha waamrisha wayapinge hayo, wala wasitake kuhukumiwa kwa hayo. Na Shetani anataka awaachishe Njia ya Haki na Uwongofu, awapotezelee mbali.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Kwani hukujua, ewe Mtume, mambo ya wale wanafiki wenye kudai kuwa wameyaamini yale uliyoteremshiwa, nayo ni Qur’ani, na yale waliyoteremshiwa Mitume kabla yako, ilhali wao wanataka kuhukumiwa, katika ugomvi unaotokea baina yao, kwa sheria ya batili, isiyowekwa na Allah Mtukufu, na wao waliamrishwa kuikataa batili? Shetani anataka kuwaepusha na njia ya haki na kuwaweka mbali nayo kabisa. Katika aya hii kuna dalili kwamba Imani ya kweli inalazimu kufuata sheria ya Allah Mtukufu na kuitumia katika kutoa uamuzi juu ya kila jambo. Kwa hivyo, mwenye kudai kuwa ni Muumini na akachagua uamuzi wa Shetani juu ya uamuzi wa Allah Mtukufu, huwa ni Mrongo katika madai yake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net