An-Nisaa 4:59
النساءيَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓا۟ أَطِيعُوا۟ ٱللَّهَ وَأَطِيعُوا۟ ٱلرَّسُولَ وَأُو۟لِى ٱلْأَمْرِ مِنكُمْ ۖ فَإِن تَنَـٰزَعْتُمْ فِى شَىْءٍ فَرُدُّوهُ إِلَى ٱللَّهِ وَٱلرَّسُولِ إِن كُنتُمْ تُؤْمِنُونَ بِٱللَّهِ وَٱلْيَوْمِ ٱلْـَٔاخِرِ ۚ ذَٰلِكَ خَيْرٌ وَأَحْسَنُ تَأْوِيلًا
Enyi mlioamini! Mtiini Mwenyezi Mungu, na mtiini Mtume na wenye mamlaka katika nyinyi. Na mkizozana katika kitu, basi kirudisheni kwa Mwenyezi Mungu na Mtume, ikiwa mnamwamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho. Hayo ndiyo bora zaidi na ndiyo yenye mwisho mwema.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Enyi mlio amini! Mt'iini Mwenyezi Mungu, na mt'iini Mtume na wenye madaraka katika nyinyi. Na mkizozana katika jambo basi lirudisheni kwa Mwenyezi Mungu na Mtume, ikiwa mnamuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho. Hayo ndiyo bora zaidi na ndiyo yenye mwisho mwema. [59]
[59] Enyi mlio sadiki aliyo kuja nayo Muhammad! Mt'iini Mwenyezi Mungu, na mt'iini Mtume, na wale wanao tawala mambo yenu miongoni mwa Waislamu wanao simama juu ya haki na uadilifu, na wanatekeleza Sharia ya Mwenyezi Mungu. Na mkizozana katika jambo baina yenu basi rejeeni kwenye Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunna ya Mtume wake ili mpate kujua hukumu yake. Kwani Yeye Mwenyezi Mungu amekuteremshieni Kitabu chake na Mtume wake amebainisha hicho Kitabu. Na katika hayo ipo hukumu ya hayo mnayo khitalifiana kwayo. Haya ni kwa mujibu wa Imani yenu kumuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho. Na haya ndio bora kwenu ili mpate kuongoka kwendea uadilifu katika mnayo khitalifiana kwayo, na mwisho wake ndio mzuri zaidi. Kwani hivyo ndio kuzuia zisitokee khilafu zinazo pelekea ugomvi na upotovu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Enyi ambao mlimuamini Allah Mtukufu na Mtume Wake na mkafuata sheria Yake kivitendo, zikubalini amri za Allah Mtukufu na wala msimuasi, mkubalini Mtume, rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie, kwa yale Aliyokuja nayo ya haki na watiini watawala wa mambo yenu isipokuwa katika kumuasi Mwenyezu Mungu. Na mnapotafautiana baina yenu katika kitu chochote, basi irudisheni hukumu yake kwenye Kitabu cha Allah Mtukufu na Sunnah ya Mtume Wake Muhammad, rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie, iwapo nyinyi mnamuamini Allah Mtukufu na Siku ya Mwisho Imani ipasavyo. Kurudisha huko kwenye Kitabu cha Allah Mtukufu na Sunnah ni bora kwenu kuliko kubishana na kusema kwa maoni, na ni mazuri kabisa marejeo yake na mwisho wake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net