An-Nisaa 4:58
النساءإِنَّ ٱللَّهَ يَأْمُرُكُمْ أَن تُؤَدُّوا۟ ٱلْأَمَـٰنَـٰتِ إِلَىٰٓ أَهْلِهَا وَإِذَا حَكَمْتُم بَيْنَ ٱلنَّاسِ أَن تَحْكُمُوا۟ بِٱلْعَدْلِ ۚ إِنَّ ٱللَّهَ نِعِمَّا يَعِظُكُم بِهِۦٓ ۗ إِنَّ ٱللَّهَ كَانَ سَمِيعًۢا بَصِيرًا
Hakika Mwenyezi Mungu anawaamrisha kwamba mzirudishe amana kwa wenyewe. Na mnapohukumu baina ya watu mhukumu kwa uadilifu. Hakika haya anayowawaidhi kwayo Mwenyezi Mungu ndiyo mazuri sana. Hakika Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kusikia, Mwenye kuona.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hakika Mwenyezi Mungu anakuamrisheni mzirudishe amana kwa wenyewe. Na mnapo hukumu baina ya watu mhukumu kwa uadilifu. Hakika haya anayo kuwaidhini Mwenyezi Mungu ni mazuri sana. Hakika Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kusikia, Mwenye kuona. [58]
[58] Hakika Mwenyezi Mungu anakuamrisheni nyinyi Waumini mrejeshe vyote mlio pewa amana, kutokana na Mwenyezi Mungu au kutokana na watu, kwa wenyewe kwa uadilifu. Basi msifanye jeuri katika kuhukumu. Haya ni mawaidha yanayo toka kwa Mola wenu Mlezi. Basi yafanyieni pupa kuyafuata. Bora ya mawaidha ni yanayo tokana naye Yeye. Hakika Mwenyezi Mungu daima ni Mwenye kusikia yasemwayo, ni Mwenye kuyaona yatendwayo. Basi anamjua anaye rejesha amana, na anaye fanya khiana, na anaye hukumu kwa uadilifu, na anaye fanya jeuri. Na kila mmoja atamlipa kwa atendalo.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Allah Mtukufu Anawaamrisha nyinyi kutekeleza aina zote za amana mlizoaminiwa nazo kwa wenyewe, msizifanyie dharau. Na Anawaamrisha muhukumu baina ya watu kwa uadilifu na uhaki, mtakapohukumu baina yao.Hilo ni jambo bora zaidi Analowaidhia Allah Mtukufu na kuwaongoza mlifanye. Hakika Mweyezi Mungu Aliyetukuka ni Msikizi wa maneno yenu, Anayajua matendo yenu na Anayaona.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net