An-Nisaa 4:57
النساءوَٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ وَعَمِلُوا۟ ٱلصَّـٰلِحَـٰتِ سَنُدْخِلُهُمْ جَنَّـٰتٍ تَجْرِى مِن تَحْتِهَا ٱلْأَنْهَـٰرُ خَـٰلِدِينَ فِيهَآ أَبَدًا ۖ لَّهُمْ فِيهَآ أَزْوَٰجٌ مُّطَهَّرَةٌ ۖ وَنُدْخِلُهُمْ ظِلًّا ظَلِيلًا
Na wale walioamini na wakatenda mema, tutawaingiza katika Bustani zipitazo mito chini yake wadumu humo milele. Humo watakuwa na wake waliotakaswa, na tutawaingiza katika vivuli vizuri kwelikweli.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na wale walio amini na wakatenda mema tutawaingiza katika Pepo zipitazo mito kati yake kwa kudumu humo milele. Huko watakuwa na wake walio takasika, na tutawaingiza katika vivuli vizuri kweli. [57]
[57] Na ambao walio yasadiki yaliyo wajia kutoka kwa Mola wao Mlezi, na wakatenda vitendo vyema, tutawalipa kwa Imani yao na vitendo vyao na tutawaingiza katika Mabustani ya Peponi yapitayo mito chini ya miti yake. Uhai wao hauna kikomo kabisa. Nao humo watakuwa na wake walio t'ahirika na kila la aibu na uchafu. Tutawapa uhai wa starehe chini ya vivuli vizuri vya kudumu, waishi maisha mema yenye neema isiyo kwisha.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na wale ambao nyoyo zao zilitulia kwa kumuamini Allah Mtukufu, kuukubali ujumbe wa Mtume Wake, Muhammad, rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie, na wakasimama imara juu ya utiifu, tutawaingiza kwenye mabustani ya Pepo ambayo, chini ya majumba yake ya fahari na miti yake, inapita mito. Watastarehe humo milele na hawatatoka humo. Watakuwa na wake humo waliotakaswa na Allah Mtukufu na kila maudhi. Na tutawatia kwenye vivuli vilivyoshikana vilivyorefuka Peponi.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net