An-Nisaa 4:56
النساءإِنَّ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ بِـَٔايَـٰتِنَا سَوْفَ نُصْلِيهِمْ نَارًا كُلَّمَا نَضِجَتْ جُلُودُهُم بَدَّلْنَـٰهُمْ جُلُودًا غَيْرَهَا لِيَذُوقُوا۟ ٱلْعَذَابَ ۗ إِنَّ ٱللَّهَ كَانَ عَزِيزًا حَكِيمًا
Hakika wale waliozikufuru Ishara zetu, tutawaingiza motoni. Kila zitakapoiva ngozi zao, tutawabadilishia ngozi nyingine ili waionje hiyo adhabu. Hakika, Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye hekima.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hakika wale walio zikataa Ishara zetu tutawaingiza Motoni. Kila zitapo wiva ngozi zao tutawabadilishia ngozi nyengine ili waionje hiyo adhabu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu na Mwenye hikima. [56]
[56] Hakika wanao pinga hoja zetu zenye kubainisha wazi wazi, na wakawakanusha Manabii, tutakuja watia kwenye Moto utakao babua ngozi zao. Na kila zikisita kuhisi adhabu Mwenyezi Mungu atawabadilishia ngozi nyengine mpya ili machungu ya adhabu yabaki yakiendelea. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye ushindi katika mambo yake, na Mwenye hikima katika vitendo vyake. Humuadhibu mwenye kumpinga na akabaki na upinzani mpaka kufa kwake. Qur'an Tukufu imeitangulia sayansi ya kisasa, ikathibitisha kuwa katika ngozi mishipa ya kuhisi, Navo, imetanda kama wavu, na hiyo hupokea mishipa yote ya kuhisi machungu, joto na baridi na mengineyo. Na hayo hayakujuulikana ila hivi karibuni.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hakika wale waliokanusha aya za Allah Mtukufu alizoziteremsha, wahyi wa kitabu Chake, dalili na hoja Zake, tutawaingiza kwenye Moto ambao watalionja joto lake; kila zikiungua ngozi zao tunawageuzia ngozi nyengine, ili adhabu yao na uchungu vipate kuendelea. Allah Mtukufu ni Mshindi, hakuna chochote chenye kumlemea, ni Mwingi wa hekima katika uendeshaji mambo Wake na uamuzi Wake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net