An-Nisaa 4:55
النساءفَمِنْهُم مَّنْ ءَامَنَ بِهِۦ وَمِنْهُم مَّن صَدَّ عَنْهُ ۚ وَكَفَىٰ بِجَهَنَّمَ سَعِيرًا
Basi miongoni mwao kuna yule aliyemwamini, na miongoni mwao kuna yule aliyemkufuru. Na Jahannamu inatosha kuwa ndio moto wenye mwako mkali.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Basi wapo miongoni mwao waliyo yaamini, na wapo walio yakataa. Na Jahannamu yatosha kuwa ni moto wa kuwateketeza. [55]
[55] Miongoni mwa walio pelekewa Nabii Ibrahim na ukoo wake wapo wenye kukiamini Kitabu kilicho teremshiwa kwao, na wapo walio kipa nyongo wakajitenga nacho. Na jaza ya hawa wenye kujitenga na wito wa Haki ni Jahannamu yenye moto wa kuteketeza.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Miongoni mwa hawa ambao walipewa fungu la elimu, kuna aliyeamini ujumbe wa Muhammad, rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie na akafuata Sheria aliyokuja nayo kivitendo. Na miongoni mwao kuna aliyekengeuka na asiitike mwito wake na akawakataza watu kumfuata. Wenye kuwatosha nyinyi, enyi wenye kukanusha, ni moto wa Jahanamu ambao utawashwa kwenu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net